Ep 31 - How Do You Move On From A Big Loss?

KIla kitu kilikua kinaenda vizuri sana kwa Gabriel, wakati akiwa anasoma chuo kikuu alibahatika kupata mwenza wa maisha. Wakajaliwa mtoto mzuri wa kiume, na baada tu ya kumaliza chuo wote wawili wakaamua kufunga pingu za maisha. Familia nzuri, na changa hii ni ndoto ya watu wengi, si ndiyo?
Lakini, wakati wa taratibu za kujifungua mtoto wa pili, mke wa Gabriel anafariki, na mtoto anapona.
Katika umri mdogo wa miaka 30, Gabriel anapoteza mwenzi wake wa maisha, na anaachiwa watoto wawili ambao inabidi awape malezi. Ni vipi anafanikiwa kuendelea na maisha yake?


Share this podcast

Continue Listening


Similar Podcasts