Ep - 21 / Self Care/ The Value of Protecting Your Energy

Hakuna mtu aliyeletwa duniani akiwa anajua kila kitu, hakuna mtu ambae ni mkamilifu wa kila kitu na hakuna mtu ambae hastahili kukua na kubadilika (Evolve and Grow)
Lakini kukua na kubadilika kwa mwanaume yeyote au mtu yeyote kunaanza pale anapojitambua na kuanza kujipenda na kujijali zaidi yeye hususani kwenye swala la afya ya akili, mwili na roho.
Mara nyingi sana jamii yetu haimpi mwanaume nafasi ya kubadilika na nafasi ya kujifunza kutokana na makosa ya nyuma au nafasi ya kubadilika na kua bora zaidi ya alivyokua jana.
Na hii ndio sababu tunataka kuzungumzia umuhimu wa “self-care” kwa mwanaume. Kwanini mwanaume ajijali zaidi yeye? Kwanini ajali ustawi wake wa afya ya akili, mwili na roho? Hii ina maana gani kwake? Inaweza kumfanya kua bora leo zaidi ya alivyokua jana?
Ungana na Michael Baruti na Nadia walipoketi na kuzungumza kuhusu umuhimu wa “self-care” kwa mwanaume pamoja na Daniel Kijo


Share this podcast

Continue Listening


Similar Podcasts