Ep 13 - Mwanaume na Familia yake vs Corona na Mambo yake

Mwezi March Mwaka 2020, Tanzania ilitangaza kesi ya kwanza ya mtu aliyegundulika na virusi vya Corona. Kwa Mussa (sio jina lake halisi) hakuona kama hili jambo linamhusu. Musa ana mke ambae ni Daktari, ana watoto wawili lakini pia anaishi na mama yake pamoja na baba mkwe wake. Pale wafanyakazi wanaofanya ofisi moja na mke walipogundulika kua na virusi vya Corona, ilimbidi Mussa aiweke familia yake yote katika “karantini”,na hapo ndipo kazi ilipoanza.
Kama mwanaume ambae ni kichwa cha familia, kwenye janga hili la Korona kila mtu anakuangalia wewe kwa majibu ya maswali yao, ili uwape uhakika kua watakua sawa. Lakini, na wewe unamuangalia nani? Nani anakupa majibu ya maswali yako? Nani anakutoa hofu? Na nani anakubali kukupa bega lake pale unapohitaji kupumzika na kusikilizwa?
Michael na Nadia wanajadili hili leo


Share this podcast

Continue Listening


Similar Podcasts