Ep 28 - Fatherhood & Parenting

Moja kati ya vipimo vya mwanaume bora kwa watu walio wengi ni namna mwanaume huyo anavyobeba majukumu yake kama baba. Lakini baba ni nani? Kazi ya baba ni nini? Baba anatakiwa awe vipi? Nini kinamfanya mtu kuwa baba bora? Nimelelewa na baba bora? Mimi ni baba bora? Nataka kuwa baba bora? Nitaweza kuwa baba bora?  Nini nifanye ili niweze kua aina ya baba ambae mwanangu anahitaji? Haya ni baadhi ya maswali ambayo wanaume wengi sana hujiuliza pindi linapokuja suala la kuwa mzazi na suala la malezi kwa ujumla. Kitu ambacho tunakifahamu ni kwamba si rahisi hata kidogo kuwa baba na ni lazima kuwekeza muda, nguvu na rasilimali.
Togolani Mavura anazungumza na Michael pamoja na Nadia kwenye “episode” hii kuhusu nafasi ya baba kwenye malezi huku akitushirikisha uzoefu na ufahamu wake wa namna ya kua baba bora na ni kwanini ni muhimu sana kwa wanaume kupokea na kukumbatia majukumu yanayokuja pindi unapoanza kuitwa baba


Share this podcast

Continue Listening


Similar Podcasts