Ep 19 - Growing up without my Mother

Mama, nani kama mama? Hakuna kama mama.
Kwa wanaume wengi, mama ndio maana halisi ya upendo. Ukiwa mtoto, mama ni mlinzi, mama ni mtetezi, mama ni muuguzi, mama ni mwalimu, mama ni kila kitu. Na ndio maana wataalam wa masuala ya akili na saikolojia wengi hua wanasema kua mara nyingi sana, mtu wa kwanza kupendwa na mtoto wa kiume anakua ni mama.
Frank, ameishi kama “mtoto wa mama” kwa miaka 14, na ghafla Mungu akaamua kumchukua mama yake. Frank aliachwa na wadogo zake wawili pamoja na baba ambae aliona kua katika umri wa miaka 14, Frank ni mkubwa wa kutosha, na ana uwezo wa kuwaangalia wadogo zake vizuri huku pia akijiangalia na yeye mwenyewe. Je, baba alikua sahihi? Ni kweli Frank alikua tayari kwa majukumu hayo? Kuondoka kwa mama kumemfanya Frank awe na mtazamo gani kuhusu maisha, mahusiano na namna ya kuishi na watu kwenye jamii?
Kwa mara nyingine tena, Michael Baruti na Nadia wanaketi na Frank kujaribu kuangalia maisha yake yalikuaje mama alivyofariki, na namna gani ameweza kukua bila mama huku wakiangalia athari yake inakuaje kwa wanaume wanaokua wakubwa bila kupata muongozo na mapenzi ya mama


Share this podcast

Continue Listening


Similar Podcasts